JINSI YA KUMSHINDA CORONA!

Mnamo tarehe 18 Machi 2020, Zanzibar tumegundua mgonjwa wa kwanza wa COVID-19. Ugonjwa huu wa mripuko umeathir mamia ya maelfu ya watu na kusababisha vifo vya zaid ya watu 15,000 duniani sasa umewasili mlangoni kwetu. Kile tulichokua tukikisoma na kukiona kwenye runinga ghafla kinagonga madirishani kwetu. Tuache ubinafsi na uwezo wa kifamilia na tuungane sote kwapamoja ili tupambane na janga hili. Imenibidi niweke huu muongozo ili kuisaidia jamii kwa kuwaasa muwe makini na kuchukua tahadhari ili kupunguza kasi ya maambukizi. Natumai hii itasaidia.

Kwanza kabisa, kila mmoja wetu asichukulie mzaha kuhusu COVID-19. Hii sio mafua ya msimu. Imeathiri maisha ya watu wengi ulimwenguni, sio tuu kiafya bali hata kiuchumi, na litaendelea kupukutisha jamii yetu iwapo hatutalipa kipaumbele. Miripuko kama hii itaathiri zaidi isipopatiwa ufafanuzi, namaanisha iwawapo tutashindwa kuidhibiti. Kwa wale waliowahi kuwa Zanzibar kwa muda mrefu, ninauhakika mnakumbuka athari za mripuko wa malaria na kipindupindu. Haya yalileta madhara kwa jamii yetu na uchumi wetu pia.


Napenda kuwakumbusha kua tunaelekea msimu wa masika. Mvua zitachangia kuzaliana kwa mbu na kusababisha malaria, dengue na chikungunya na marakwamara tunaona ongezeko la kipindupindu na taiphoidi katika kipindi hichi. Kitu cha mwisho tunachohitaji kipindi hiki cha mvua ni huyo kirusi mpya anaechafua hali ya hewa kila mahala aendapo. Wengine mtadhani kua watu wenye COVID-19 wanadhofu tuu kidogo kwaio sio tatizo kubwa na kusema tuendelee tuu na maisha yetu, na maelezo haya yote kuhusu machafuko ni matishio tuu ya “vyombo vya habari “. Kwakua watu wengi wanaopata maambukizi ya kirusi hicho wanaendelea vizuri kwa wale walionaumri mdogo na afya bora. Kwaio tatizo likowapi, si ndio? Sawa, kwasababu asilimia ndogo ya watu walioathiriwa zaidi na maabukizi haya ya COVID-19 ni wale wenye umri mkubwa kwanzia 60 na wagonjwa wengine (lakini wadogo na walio na afda nzuri pia WANAWEZA kuumwa sana). Hii inamaanisha wazazi wetu, mabibi na mababu zetu, majirani, marafiki, nk. Asilimia ndogo hii ya watu tunaweza kusema ni idadi ndogo tuu, lakini takribani familia za watu 16,000 ulimwenguni wamepoteza wapendwa wao miezi michache ilopita. Lakini pia COVID-19 inaweza kutuyumbisha kiuchumi.


Kwanjia nyingi hili linaweza kutuathiri sote, sio tuu watoa huduma za afya, lakini pia walio masikini ndio watateseka zaidi. Watu masikini hawana hakiba kifedha pindi shuhuli zote za kijamii zikizuiliwa. Hawana uwezo wa kumudu kununua chakula kingi cha hakiba na pia hawana uwezo wa mambo mengi kama wengine walionao kifedha. Mbali ya kugundulika na kuthibitishwa kwa muathirika huyo Zanzibar hadi sasa, sisi binafsi tunatakiwa kuchukua tahadhari ilituweze kirusi katika shuhuli zetu za kilasiku kimaisha kwa kufuata muongozo ufuatao.

Muongozo wa kuepuka janga la COVID-19 

  •  USIOGOPE.kupata maambukizi ya “coronavirus” au COVID-19 sio mwisho wa dunia. Watu wengi wamepona na wanaendelea vizuri.

  •  FANYA SEHEMU YAKO. Hii sio vita ya serekali tuu, ni yetu pia. Sote tunatakiwa kufanya sehemu yetu kwa kueka mazingira kwenye hali ya usafi kwa “kukohoa kwenye visigudi vyetu” au “mbali na eneo la watu”, hii haimaanishi kutotembelea marafiki, lakini inamaanisha kujitenga na kuishi na familia yako tuu. Isipokua tuu ukiwa kazi yako hairuhusu kubaki nyumbani, lakini pia uepuke mikisanyiko ya watu.

  • ONGEZA KINGA YAKO YA MWILI. Tumia muda huu kutengeneza afya yako, hii inamaanisha kuongeza vitamini C mwilini (tunaishi katika kisiwa kijichojaa matunda) ule chakula kilichobora kiafya na kulala walau masaa 8 kwa siku, kunywa maji ya kutosha walau gilasi 8 na kufanya mazoezi ya mwili walau dakika 150 katika juma. Na kupunguza kupokea kila tunachokisikia katika mitandao ya kijamii ingawa ndo tunapopata habari ila muda mwengine watu wanazidisha habari zisizo na ukweli.

  • ISHI KIAFYA. Hii ni pia kuukinga mwil wako, usisahau maadui wetu wa sikuzote kama malaria, chikungunya dengue, taiphodi na kipindupindu. Tumia vyandarua vyenye dawa za mbu, dawa za kuulia mbua pia uoshe mikono yako mara kwa mara na epuka kula mbogamboga mbichi mitaani au sehemu zisizo rasmi. Na kumbuka kupata virutubisho vya vitamini D.

  • KATISHA KUSAFISI. Tunaelewa kuna baadhi ya watu wanajihisi wapo salama wakio nchini mwao na kwahio wanataka warudu ili kua na famlia zao. Hii inaeleweka ila tunawashauri wasafiri wote kuchukua tahadhari kupindi cha safari zao. Na pia kuwashauri watu wanaotaka kuitembelea Zanzibar kua wasitishe safari zao hadi mwezi wa 6 ambapo kilakitu kinatarajiwa kua sawa na hali kua ya usalama (INSHALLAH).

  • BAKIA NYUMBANI. Ikiwa inajihisi kua na dalili ya maambukizi au za ugonjwa huu, hushauriwi tuu kukimbilia hospitalini lakini kwanza fuata njia za awali za ugonjwa huu kwa kujitenga pekeako na kula kama inavyoshauriwa zaidi matunda yenye vitamini C, maji mengi. Lakini kwa zaidi ukiona sasa hizi ndizo dalili za ugonjwa huu piga simu kituo cha dharurua au tembelea kituo cha afya kilichopo karibu nawe ikiwa unachukua tahadhari ya kuwaambukiza wengine kwa kuwapa taarifa juu ya afya yako au weke miadi yako nasi hapa.

  • USAFI WA MIKONO. Kosha mikono yako kwa maji na sabuni ndani ya sekunde 20 au tumia sanitizer ya kuisafishaia mikono. Hii ni kwasababu kwakila tunachokifanya tunatumia mikono yetu na ndio njia kuu ya kusambaza vizrusi vya ugonjwa huu, wasiliana nasi ikiwa unahitaji semina kuhisiana na elimu ya afya ya mazingira dhikinmaambukizi ya corona katika jamii yako.

  • KUA NA BUSARA. Ni jambo ambalo sote hatujalizowea. Ni kirusi kipya ambacho tuna taarifa zake kidogo tuu. Hiki ni kipindi kigumu kwetu sote ila inatupasa kua wavumilivu na kuheshimiana. Tuisaidie jamii yetu na serekali na wote wanaotoa jitihada zao kulishuhulikia tatizo hili. Tupo katika hili sote kwapamoja.

  • KUA MTULIVU. Jipumzishe na tumia muda huu kujitafakari. Jaribu kufanya mambo mapya , kuandika vitabu au kuvumbua mapishi mapya. Furahia na wapendwa wako na tengeneza maji ya malimau unywe kutoka katika milimau ambayo dunia inatupatia.

  • KUJITENGA MBALI NA JAMII. Japokua nimeliongelea hili huko juu. Ila ningependa kuligusia tena. Huu sio wakati wa mitoko ya chakula cha usikua au sherehe za kukesha. Ndio itatuuwia vigumu kwa kipindi hiki lakini tutakua hatarini zaidi iwapo tutazembea, tutukitolea nje mfumo wa kisaikolojia na kiuchumi. Kama unatumia usafiri wa umma, weka dhana ya ku kuna muathirika wa COVID-19 na uchukilie tahadhari zote. Jaribu kupanda dalala ukiwa na pesa taslimu ya kulipia nauli kuliko kupokea pesa iliyotoka kwa mtu mwengine ndani humo na uvae maski ukiwa kwenye hadhara ya watu. Safisha mikono yako vizuri zingatia kutoshika vitu vyako baada ya kuosha mikono bila kuvisafisha (hat simu yako ya mkononi pia). Hakikisha unasafisha kila kitu chako ndipo ukitumie. Kua makini unapokua karibu na watu wenye dalili zote za ugonjwa kwa kua ni jukumu letu kujilinda na kuilinda nchi yetu.

Thank you Kawthar Buwayhid of the International School of Zanzibar and Agnes of WAJAMAMA Wellness Center for helping me translate this document!

Previous
Previous

Deliveries and Curb-Side Pick-Ups

Next
Next

WAJAMAMA’s  COVID-19 Survival Guide